UBUNIFU: Hii ndio njia mbadala ya kuepukana na uchimbaji wa mashimo kwa sungura hasa kwa wale wafugwao katika maeneo ya wazi Mf: chumba.


Wafugaji wengi wa sungura wanaofuga katika maeneo ya wazi mfano chumba, bustanini hulalamika sana suala la sungura wao kuchimba mashimo na kukaa ndani ya mashimo kwa muda mwingi halikadhalika kuzalia huko huko. Kwa kuwa baadhi ya sungura hupendelea kuchimba kutokana na mazingira waliyopo ni vyema mfugaji kuwa mbunifu kwa kuwatengenezea mabanda yenye baadhi ya sehemu zenye muundo wa mashimo either kwa kutumia mabomba au kuchimba ardini na kuweka wavu ambao umetengenezwa kwa muundo wa mviringo na katikati kunakuwa na uwazi ambapo sungura anaweza kupita na kuhisi furaha kama anavyokuwa katika mashimo.


Image result for wavu za sunguraImage result for bomba kubwa za maji
na kufanya hivyo ni ili kuepukana na majanga yanayojikoza mara kwa mara kama panya/paka/nyoka kuwala watoto wa sungura huko katika mashimo pindi sungura jike anapozalia katika mashimo.

Halikadhalika kufanya hivyo ni kuwaweka sungura wako katika mazingira salama wakati wote.
Ni baadhi tu ya faida za ubunifu huu katika ufugaji wa sungura ili kuwaweka sungura wako katika mazingira salama.
  Asante, na Karibu

0 comments:

Post a Comment