Hizi ndizo aina maarufu za sungura zinazofugwa kwa wingi nchi Tanzania.















Kutokana na upelelezi uliofanywa na moja ya team inayounga mkono harakati za kimaendeleo katika secta ya ufugaji wa sungura Tanzania umebaini kwamba sungura wanaopendelewa kufugwa zaidi nchini Tanzania ni kama vile
 
Hawa ni White Newzealand Rabbits ndio sungura namba moja wanaoongoza kwa kufugwa nchini Tanzania kulingana na upelelezi uliofwana na Usbm team.  Sungura hawa huzaa kwa kiwango kikubwa ambapo huweza kuzaa watoto 6 hadi 12 na hubeba mimba kawa siku 29 hadi 31 kulingana na matunzo na afya yao.
Pia huvutia sana hasa kwa rangi yake nyeupe ya kupendeza halikadhalika ni wapole.



Hawa ni Californian Rabbits , pia sungura hawa hufugwa kwa wingi sana nchini Tanzania. hawa huwa weupe mwili mzima isipokuwa kwenye  kichwa, masikio na  miguu huwa weusi. pia huvutia sana machoni hasa kwa rangi yake ya kuvutia nyeupe na nyeusi hivyo huwavutia watu wengi sana hutamani kuwafuga hata kwa kuwa mapambo majumbani mwao.
Halikadhalika hawa hubeba mimba siku 29,30 hadi 31 kulingana na afya yake.etret





Aina hii hujulikana kwa jina la Chinchilla pia sungura hawa hufugwa kwa wingi sana nchini Tanzania jike hubeba mimba siku 29 hadi 31 huwa na umbo kubwa na mwili mkubwa tofauti na White newzealand rabbits na Californian rabbits, huwa na rangi zuri  na ya kupenda ukiitazama uanona kamba kijivu na nyeupe na nyeusi mchanganyiko halikadhalika huwa na masikio makubwa yenye kusimama juu, pia sungura hawa ni wakorofi sana hasa wanapochangwanywa madume kuanzia wawili na kiuendelea katika sehemu moja huwa wanang'atana :Angalizo: unapowafuga sungura hawa ni vyema ukawatenganisha madume ili kuepukana na athari zitakazo jitokeza mbeleni kwa sababu kinga ni bora kuliko tiba hivyo bora kuchukua angalizo mapema kabla ya madhara kutokea na kukufanya ukakata tamaa ya kufuga kwa sababu ndogo ndogo kama hizi.
 Asante naimaini utakuwa umejifunza.

0 comments:

Post a Comment