Mambo ya kuzingatia kabla hujaanza kufuga sungura kisasa kwa manufaa ni yafuatayo





 











 Kwa kawaida mtu anapotaka kufanya jambo ni lazima afikirie ataanzaje na ili apate mwanzo mwema hivyohvyo pia unapofikiria kufuga sungura ni lazima ufikiri je nitaanzaje, nitatumia nini, nitapata wapi , na nikipi hicho nitachoanza nacho ili kufikia malengo unayoyatarajia
Hivyo bhasi haya ni baadhi ya mambo ambayo unapaswa unayatambue na kuyazingatika kabla ya kuanza kufuga sungura.
1. Aina ya sungura.
     Ni muhimu kufikiria ni aina gani ya sungura ambao ukiwafuga watakuletea manufaa hasa kwa  ufugaji ulio bora.
2. Banda la sungura.
     Ni muhimu pia kuzingatia uchaguzi wa mabanda ya sungura ya kisasa  na yenye usalama wa kutosha kwa sungura wako Note; hakikisha usitumie mabanda ya vioo sio mazuri kwa usalama wa sungura wako kwa kuwa hayapitishi hewa  kwa wingi kwa sungura wako ni vyema kutumia mabanda ya mbao au wavu mfano wavu wa kuku..
3. Kuwa na nia ya kufuga sungura.
      Hakikisha kweli umeamua kufuga sungura na unapenda kufuga sungura.
3. Elimu ya ufugaji/ujuzi.
      Halikadhalika unapoamua kutaka kufuga sungura hakikisha umepata elimu juu ya ufugaji wa sungura ili uweze kufuga vizuri na kisasa kwa kutambua changamoto za ufugaji wa sungura ili pia ujue ni jinsi gani utakabiliana nazo pindi utakaopokutana nazo.
4. Sehemu ya kufugia.
         Pia ni vyema kuwa  na eneo la kufugia na je ni salama kwa sungura wako endapo ukianzisha ufugaji katika eneo hilo 
5. Mtaji.
        Ni muhimu pia kuwa na mtaji wa kuanzisha ufugaji huo maana kama mnavyotambua hakuna kitu kisicho na gharama hivyo bhasi mtaji unahitajika katika kufanikisha hili na ufugaji wa sungura hauitaji gharama nyingi na kubwa ili kuanzisha mradi huu bali huitaji mtaji mdogo tu.
6. Upatikanaji wa chakula cha sungura.
       Pia ni muhimu kutambua ni jinsi gani utapata chakula cha sungura kama majani, pumba na vingine unavipataje na ni wapi utavipata vyakula hivyo ili utakapoanzisha mradi uwe na uhakika na unatambua upatikanaji wake.
    asante. 

0 comments:

Post a Comment