Historia ya kisiwa chenye mamilioni ya sungura kiitwacho "Rabbits Island kilichopo katika Bahari Inland ya Nchini Japani.







Rabbits Island  Ni kisiwa kidogo katika Bahari ya Inland ya Japani ina historia ya kuvutia, Kati ya mwaka wa 1929 na 1945, Kisiwa cha Okunoshima kilikuwa kisiwa cha uzalishaji wa sumu ya gesi kwa ajili vita  kwa  Jeshi la Kijapani la Imperial ambalo lilizalishwa zaidi  za gesi hizo.
Kisiwa hicho kilikuwa na jukumu muhimu  la uzalishaji wa sumu ya gesi kwa ajili vita  kaw wanajeshi wa japan wakati wa Vita Kuu ya II kwa siri. Na Kwa sababu ilikuwa ikitengeneza silaha ya kemikali ambazo zilikuwa zimepigwa marufuku chini ya mkataba wa kimataifa, kisiwa hicho kilifutwa kwenye ramani rasmi. Kisiwa hiki kilichaguliwa kutokana na jiografia yake kuwa inaruhusu viwanda  kwa sababu ilikuwa mbali na Tokyo Japan ili kutoleta madhara kwa watu wake.

Wakati huo waukoloni walikuwa wakiwatumia sungura  katika kisiwa hicho ili kupima madhara ya sumu wanayoitengeneza. Siku hizi, kisiwa hicho kimekuwa nyumba ya sungura ambapo huwa kama kivutio kwa watalii nchini humo.

 Unapofika katika kisiwa hicho gharama ya feri ni JPY 620 ambayo ni sawa na shilling  12,518.77 za kitanzania kwa safari ya pande zote na safari  inachukua takribani dakika 10 tu hadi kufikia kisiwa hicho.



Kabla ya kuelekea kwenye kisiwa hicho unaweza ukanunua chakula cha sungura ili kwenda kuwapatia sungura pindi  unapohitaji kufurahi nao kwa kuwapatia taratibu ili uweze kucheza nao kwa muda mrefu.

Na inavyosadikika katika kisiwa hicho Rabbits island hutoweza kununua chakula cha sungura kwenye kisiwani humo kwa kua hakuna vyakula kisiwani hapo. Pia unaweza kununua vyakula kwa ajili yako mwenyewe, kwa sababu kisiwani hakuna migahawa ya kupata chakula.

Kwa kuwa kisiwa hicho kuwa maarufu sana nchini humo hivi karibuni, kuna wageni wengi sana kwenye kisiwa hicho. Hivyo kunakuwa na foleni kwa takribani muda wa dakika 30 wakati  kununua tiketi na kisha upande kivuko. Hasa mwishoni mwa wiki na likizo za kitaifa kunakuwa na watu wengi sana.

Na unapohitaji kutembelea kisiwa hicho ni vyema kuwahi mapema kama saa 8 asubuhi. Ili uepukane na usumbufu utakao jitokeza mfano foleni kutokana na makundi ya watalii na pia mda huo sungura huwa bado wana njaa sana Kwa maana kwa mida ya mchana sungura wanakuwa wameshiba na kufanya hivyo ni ili kuenjoy na sungura kwa muda mrefu kwa kuwadanyia na chakula kama carrot,kabegi na n.k








Halikadhalika Taadhari zinatolewa kwa wageni kwa kutowalisha sumu au vitu vilivyohatari kwa maisha yao sungura hao wapatikanao katika kisiwa hicho. Kwa maana katika kisiwa hicho kuna mamilioni ya sungura na wa aina tofauti tofauti na wakupendeza sana machoni.

Pia katika kisiwa hicho ukiachana na sungura pia kuna masalia ya majengo ya viwanda vya kutengenezea gesi ya sumu zilizotumiwa na wanajeshi kipindi cha ukoloni..


Asante na kariribu .




0 comments:

Post a Comment